Jumanne 8 Julai 2025 - 21:57
Waislamu wa Georgia wakiwa wamebeba picha za Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi, wametangaza mshikamano wao na Taifa la Iran

Hawza/ Imamu wa jamaa wa Msikiti wa Imam Ali (as) wa Marneuli, katika maandamano ya siku ya Tasu'a na Ashur'a ya Husein (as) ya Waislamu wa Kishia wa Georgia alisisitiza kuwa: Waislamu wa nchi hii wamesimama “kwenye upande wa haki na upande wa waliyu Faqihi”.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza likinukuu kutoka katika Umoja wa Redio na Televisheni za Kiislamu, maandamano ya hamasa ya Waislamu wa Kishia wa Georgia katika siku ya Tasua na Ashura ya Imam Husein (as) yalikuwa ni tukio lisilo na mfano wa kuonyesha mapenzi na mshikamano wao kwa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi, kwa mara ya kwanza picha za Ayatollah al-‘Uẓmā Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, zilipandishwa kwa fahari miongoni mwa waombolezaji wa Husein katika nchi hiyo.

Maandamano haya yalikuwa ni ujumbe wa wazi wa ulinganifu na ufuasi wa Waislamu wa Kishia wa Georgia kwa nafasi ya "Wilayat al-Faqih", katika muktadha huo, Hujjat al-Islam Hajji Hajjiov, imamu wa jamaa Msikiti wa Imam Ali (as) katika mji wa Marneuli, katika hotuba aliyotoa mbele ya washiriki wa maandamano hayo alisisitiza juu ya mshikamano huo.

Hajjiov katika hotuba yake alisema: “Hatuna shaka yoyote kuwa tuko upande wa haki na upande sahihi wa historia; tuko upande wa waliyu Faqihi.”

Maneno haya yanaonyesha msimamo thabiti na wa wazi wa Waislamu wa Kishia wa eneo hilo katika kuunga mkono "Wilayat al-Faqih" na Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha